Pictures

VIDEOS

TAARIFA YA BAADHI YA MATUKIO YA UBALOZI WA NEW YORK

Mwezi wa November’s 2017 Baadhi ya Mabalozi Wawakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa wa nchi ambazo ni marafiki wa Canada walipewa Mwaliko Na Mh. Waziri Mkuu wa Canada Mh. Justin Trudeau ili kuzungumzia masuala ya utunzaji Amani Duniani kwa kutoa vikosi vya ulinzi vya Usalama Na nyenzo mbadala katika nchi zenye migogoro. Vile vile walizungumzia masuala ya Amani Afrika, Mashariki ya kati na changamoto ya Korea ya Kaskazini. Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa alipata fursa ya kufanya mazungumzo ya faragha Na kiongozi huyo ili kunadi fursa za nchi Jijini Vancouver kwa kumpa Salam kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mh. Dr. John Pombe Maghufuli Na kumweleza shukrani za Mh. Rais kwa misaada yote ya nchi yake kwa Tanzania. Vilevile nilipata fursa ya kumweleza Shauku ya Tanzania kukuza zaidi mahisiano katika nyanja za uwekezaji kwenye viwanda, kilimo, teknolojia na sekta za Afya Na elimu. Mh. Waziri Mkuu huyo alikiri uhusiano wetu mkubwa wa kihistoria Na lengo lake la k kuza uhusiano huo na kuendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali.

t2

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Cambodia Mh. Ry Tuy Umoja wa Mataifa Aliutembelea Ubalozi wetu New York mwezi wa februari 2018 Na kuonesha kufurahishwa Na taarifa ya maendeleo ya Kasi ya uchumi wa Tanzania. Tulipata wasaa wa kubadilishana mawazo hususan katika Nyanja za maendeleo ya uchumi na viwanda kwa nchi za kusini mwa dunia na kumueleza nia ya kukuza mahusiano yetu. Mheshimiwa Balozi huyo Aliahidi kuishauri nchi yake kuanzisha mahusiano ya kiuchumi Na biashara hatimaye kuanzisha Ubalozi Tanzania. Amefurahishwa sana Na hatua za Serikali ya awamu ya tano kama anavyosoma katika vyombo vya habari.

t3
t4

Waziri wa Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Balozi Dakta Augustine P. Mahiga akifuatilia hotuba za nchi Mbalimbali katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani Septemba 2017. Mheshimiwa Waziri alitoa hotuba yake ambayo ilisheheni masuala ambayo yaliungwa mkono na nchi nyingi na kuomba nakala ya hotuba yake.

t5

Baadhi ya Mabalozi Na Wawakilishi wa Kudumu Umoja wa Mataifa wa nchi rafiki za Kiafrika walikaribishwa Na Serikali ya Ujerumani ili kujadili masuala ya ushirikiano na utunzaji wa Amani na masuala ya ushirikiano wa maendeleo katika suala la maendeleo endelevu. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Kiongozi Mkuu wa Serikali ofisini kwake Berlin. Tulipata picha ya pamoja na Mheshimiwa – Chancellor Angela Merkel ofisini kwake. Serikali ya ujerumani imeonesha nia thabiti ya kuendelea kushirikiana Na serikali za Afrika katika Nyanja za uchumi, usalama na amani ikiwemo maendeleo ya watu.

t6

Sherehe ya MUUNGANO wa Tanzania Na Zanzibar New York kwa kushirikiana Na Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania.

Mayor mstaafu wa Jiji la New York Michael Bloomberg ambaye ni mmoja wa matajiri 10 wa Duniani hunishirikisha katika mikutano yake yeye akiwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Kamati yake ya Kimataifa ya Majiji endelevu yanayozigatia mazingira na kuweka miji safi, salama yanayozingatia mabadiliko ya hali ya hewa. Picha hii akiwa Na Mh. Balozi Modest Mero Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa. Mayor Bloomberg ameahidi kuendelea Na misaada yake Tanzania katika sekta ya Afya ya uzazi wa kina mama na watoto jambo ambalo alilianza kwa kushirikiana Na Rais Mstaafu Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

t8
t9

Balozi Modest Mero akiwa na majadiliano na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kujadili mchakato wa kuboresha utendaji wa Umoja wa Mataifa katika maeneo ya Usalama Na Amani, Mfumo wa Uendeshaji vyombo vya maendeleo Duniani (UN Development System) pamoja na kuboresha mifumo ya utendaji ya UMOJA WA MATAIFA

Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa tulikaribishwa na Serikali ya Israel ili kujionea wenyewe hali ya Usalama ya nchi hiyo ikiwemo mahusiano ya kiuhasama na Wapalestina. Tulipata pia fursa ya kushirikishwa katika sherehe za uhuru za nchi hiyo miaka 70 ikiwemo kuoneshwa maeneo yenye migogoro na kutokuwa na usalama. Picha hii ya Pamoja tulipiga tukiwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Benjamin Netanyahu. Katika mazungumzo na Mh. Waziri Mkuu alieza nia yao ya kushirikiana na Tanzania katika maeneo ya kilimo teknolojia ya umwagiliaji na nishati ya jua. Vilevile watashawishi wawekezaji katika viwanda ili kukidhi lengo la Tanzania la kujenga viwanda.

INAWASILISHWA  10 MAY 2018,
UBALOZI NA UWAKILISHI WA KUDUMU
NEW YORK

t10